Luke 10:25-30

25 aWakati huo mtaalamu mmoja wa sheria alisimama ili kumjaribu Isa, akamuuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

26Isa akamjibu, “Imeandikwaje katika Torati? Kwani unasoma nini humo?”

27 bAkajibu, “ ‘Mpende Bwana Mwenyezi Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote’; tena, ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ ”

28 cIsa akamwambia, “Umejibu vyema. Fanya hivyo nawe utaishi.”

29 dLakini yule mtaalamu wa sheria, akitaka kujionyesha kuwa mwenye haki, akamuuliza Isa, “Jirani yangu ni nani?”

30Isa akamjibu akasema, “Mtu mmoja alikuwa akiteremka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko, naye akaangukia mikononi mwa wanyang’anyi. Wakampiga, wakaondoka, wakamwacha akiwa karibu kufa.
Copyright information for SwhKC